
Paul Clement amesema kuwa Sergio Ramos, nahodha wa Chelsea John Terry na beki wa Paris Saint-Germain Thiago Silva ndio mabeki bora wa kati kwa sasa ulimwenguni.
Ramos amekuwa akihusishwa kujiunga na Mashetani Wekundu Manchester ikiwa kama Madrid nao watamchukua mlinda mlango wao David de Gea
Clement, ambaye amewahi kuwa kocha wa Madrid kabla ya kujiunga na klabu ya Derby County msimu huu wa majira joto, amesema kuwa Ramos ni moja ya mabeki bora kabisa wa kati ambao amewahi kuwashuhudia.
"Ni mchezaji mzuri sana, ni moja kati ya wachezaji bora sana ambao nimewahi kuwafundisha," Clement aliiambia Sky Sports. "Ana ubora wa hali ya juu sana, ni mchezaji wa ajabu, kiongozi, mshindani, mwanamichezo, kwa ujumla ni mchezaji wa aina yake.
"Ni moja ya mabeki bora wa kati kwa sasa ulimwenguni - na nimewahi kufanya kazi na baadhi wazuri kama yeye, mfano; Terry, Thiago Silva wa PSG, Pepe, Raphael Varane lakini kwa kiasi fulani Ramos yuko juu ya wote hao, alisema
0 comments:
Post a Comment