Wakati Chile wakijiandaa kuwakabili Argentina kwenye fainali ya Copa America itakayopigwa ulisiku wa leo (Jumamosi) kuamkia kesho (Jumapili), kikubwa zaidi katika maandalizi hayo ni namna ambavyo kocha wa Chile amekuwa akiwaandaa wachezaji wake kwa kutumia game la mpira (PlayStation) kwa ajili ya kumdhibiti nyota wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi.
Kocha wa Chile Jorge Sampaoli amesema: “Tumekuwa na utaratibu wa kutumia teknolojia ya PlayStation na tutahamishia uwanjani kila tunachojifunza. Tumewaambia wachezaji tutatumia mfumo wa 4-4-2 na tayari game hilo limeshatuonesha ni kwa jinsi gani mfumo huo utafanyakazi dhidi ya wapinzani wetu.


Sampaoli amepanga kuwatumia Gary Medel, Francisco Silva na Eugenio Mena kama walinzi wa kati huku Marcelo Diaz na Cherle Aranguiz wakicheza kama kama walinzi wa pembeni wakati Aturo Vidal, Mauricio Isla na Jean Beausejour watacheza kama viungo nyuma ya Eduardo Vargas na Sanchez watakaocheza kama washambuliaji.


Lakini pia tunatakiwa kutambua kuwa, Argentina inawanawachezaji wengine wazuri. Tunatakiwa kuwa waangalifu kwao na sio kwa Messi pekee. Argentina wamecheza vizuri kama timu kwenye mashindano haya lakini tunatakiwa kuwashinda.
0 comments:
Post a Comment