NAHODHA wa Azam fc, John Bocco ‘Adebayaor’ amezungumzia
mechi ya kesho kutwa jumatano dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
“Yanga ni timu nzuri, lakini kumbuka sisi ni wanajeshi,
tunakwenda kupambana nao kwa nguvu zote na kupata pointi tatu. Nafasi ya pili
lazima tuchukue, tumefungwa na Simba (2-1), mechi ilikuwa ngumu, lakini nadhani
kadi nyekundu (Salum Abubakar) ilituharibia mpango wa mechi, ilikuwa mapema na
tumecheza pungufu kwa muda mrefu. Hata hivyo tumecheza vizuri, tunajiandaa na
mechi ijayo dhidi ya Yanga na ile ya Mwisho na Mgambo JKT”.
0 comments:
Post a Comment