Tuesday, August 30, 2016

Kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 12 cha klabu ya  Barcelona mwishoni mwa Juma lililopita kilitwaa Ubingwa wa mashindano ya vijana nchini Japan kwa kuwachapa bao 1-0 wenyeji Omiya Ardija Junior, lakini kinachogonga vichwa vya habari kwasasa sio matokeo ya mechi hiyo.

Kupitia mtandao wao wa Twita, Barcelona wame-post video yenye maneno yanayosomeka FairPlay yaani mchezo wa kiungwana ambayo  inawaonesha vijana wake wakiwafaraji vijana wenzao wa Omiya baada ya kuwaburuza na kupoteza kombe wakiwa kwenye ardhi yao.

Baada ya kuwachapa Wajapan hao, nyota hao wa miamba ya soka la Hispania, Barca, walimtia moyo kila mchezaji wa timu pinzani ambapo wengi wao walikuwa wakimwaga machozi.

Tendo hilo la upole liliongozwa na Nahodha wa Barcelona Adria Capdevila Puigmal – na sasa limewagusa mashabiki wa kandanda Duniani kote.

 Barcelona walioshinda mabao manne kwa bila dhidi ya Ventforet Kofu mechi ya ufunguzi, halafu nusu fainali  wakachomoza na ushindi kama huo mbele ya Tokyo Verdy Junior , walijikuta wakipata wakati mgumu zaidi kwenye mechi ya fainali ambapo walishinda kwa mbinde goli moja kwa Nunge na baada ya kipyenga cha mwisho waliwapongeza wapinzani wao kwa kiwango kikubwa walichoonesha.

Kitendo hiki kilikumbushia namna nahodha wa zamani wa Barcelona,   Xavi alivyomfariji Andrea Pirlo baada ya Barca kushinda mabao matatu kwa moja katika fainali ya  ligi ya mabingwa Ulaya mwezi Juni 2015 mjini Berlin, Ujerumani.


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video