BAADA ya kufungwa na Simba magoli 2-1 jana uwanja wa Taifa,
kocha mkuu wa Azam fc, Mganda, George ‘Best’ Nsimbe amesema hayo ni matokeo ya
mpira na wanajipanga kwa mechi ya kesho kutwa dhidi ya Yanga itayopigwa uwanja
wa Taifa.
“Ni matokeo ya mpira, tumepata nafasi nyingi tumetumia moja,
wenzetu wamepata nafasi mbili wametumia zote, lakini nafasi ya pili lazima
tuichukue. Naye refa alituua kwa kumpa kadi nyekundu mchezaji wetu (Salum
Abubakar), tunakwenda kucheza na Yanga, halafu mechi ya mwisho tutacheza na JKT
Ruvu, lazima tuvune pointi zote” Amesema Nsimbe.
0 comments:
Post a Comment