Sunday, May 3, 2015

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans wanatarajia kuwasili kesho jijini Dar es salaam majira ya saa 8:00 mchana kwa ndege ya Emirates.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema msafara wa Yanga unaondoka leo nchini Tunisia na utapitia Dubai na kutua Dar es salaam.
"Kinachoendelea hapa Tunisia ni kufungasha virago vyetu, tunaondoka leo kupitia Dubai, kesho tutawasili Dar es salaam majira ya saa 8:00 mchana". Amesema Muro.
Licha ya kutolewa na Etoile Du Sahel kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1, Jerry Muro amesema uongozi umeridhisha na kiwango ambacho vijana wao walionesha na wanarudi nyumbani kuendelea na ligi kuu, lakini mwakani watarejea tena katika michuano ya kimataifa kwani wao ni 'wakimataifa zaidi".
Yanga ilifungwa goli 1-0 jana mjini Sousse Tunisia na mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam majuma mawili yaliyopita, timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video