GAZETI la Ufaransa la French daily L’Equipe limeripoti
leo kuwa Manchester United wamewasiliana na mlinda mlango wa Tottenham Hotspurs, Hugo Lloris kuhusu kumsajilimajira ya kiangazi.
United wanavutiwa na Lloris wakati huu wakitarajia kumuuza David De Gea kwenda Real Madrid.
Kwa ufupi, De Gea anaondoka Old Trafford majira ya kiangazi mwaka huu na Mashetani wekundu wametupia macho yao kwa Lloris kama mrithi wa Mhispania huyo.
Ripoti ya L'Equipe inasema mshauri wa Hugo amevujisha stori hiyo kwa lengo la kuwapa presha Spurs.
Gazeti hilo pia limeandika kwamba Lloris pia anawindwa na Real Madrid kama dili la De Gea litashindikana.
Wiki kadhaa zilizopita, ilitoka ripoti ya utata kuwa Lloris anaweza kuvunja mkataba na Spurs kama watashinda kufuzu ligi ya mabingwa mwakani.
Hugo Lloris bado amebakisha miaka minne katika mkataba wake na Tottenham.
0 comments:
Post a Comment