Msemaji wa Simba, Hajji Sunday Manara
SIMBA wasipopata nafasi ya pili msimu huu wataendelee
kutoshiriki michuano ya kimataifa barani Afrika kwa mwaka mwingine tena.
Hili litakuwa pigo kwa klabu hii kongwe nchini na mara ya
mwisho kucheza ligi ya mabingwa ni mwaka 2012 walipochukua ubingwa msimu wa
2011/2012 chini ya kocha mserbia Milovan Circovic.
Msimu wa 2012/2013 Yanga walichukua ubingwa, Azam walishika
nafasi ya pili na Simba wakashika nafasi ya tatu, hivyo wakakosa kushiriki
michuano ya kimataifa.
Msimu wa 2013/2014 Azam fc walichukua ubingwa, Yanga
wakashika nafasi ya pili, hali ikawa mbaya zaidi kwa Simba kwani waliishia
nafasi ya nne wakizidiwa na timu mpya ya Mbeya City iliyochukua nafasi ya tatu.
Msimu huu kuna asilimia kubwa kwa Simba kushika nafasi ya
tatu, ya pili ikishikwa na Azam fc wakati Mabingwa tayari ni Yanga.
Wapenzi wa soka hasa mahasimu wao Yanga hawataki kuona Simba
ikishika nafasi ya pili na kupanda ndege kushiriki michuano ya Afrika.
Ukienda uwanja wa Taifa, mashabiki wa Yanga wanakuwa na
mabango yanayosema Simba wataendelea kupanda boti za Azam kwenda kuweka kambi
Zanzibar. Hizo ni kejeli za watani wa jadi na ni za kawaida katika soka.
Lakini Simba wao wanasemaje kuhusu umuhimu wa kupanda ndege
msimu ujao au kutopanda ndege kushiriki michuano ya Afrika?
Afisa habari wa Simba, Hajji Sunday Manara ametoa kauli hii:
“Kupanda ndege sio ishu kwasababu hata mizigo inapanda ndege, ishu hapa ni
kushinda mechi ya Azam leo, unaweza kupanda ndege halafu unatia aibu, unapigwa
nane, sita, ina maana gani sasa?”
Kabla ya Yanga kucheza na Etoile du Sahel jana na kutupwa
nje kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1 baada ya kufungwa 1-0 Tunisia na kutoka
sare ya 1-1 uwanja wa Taifa Dar es salaam, Manara alisema kama Yanga wataifunga
Etoile basi atatembea uchi kuelekea jangwani kwenda kuwapigia magoti na kuwapa
shikamoo.
Sasa Hajji amenusurika kutembea uchi baada ya Yanga
kushindwa kupata matokeo mazuri.
0 comments:
Post a Comment