Wednesday, January 11, 2017

Na Samuel Samuel
Mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi kati ya Yanga SC na Simba SC umemalizika kwa mikwaju ya penati na mnyama Simba SC akiibuka kidedea kwa kupata 4-2.
Kwa ujumla ni moja kati ya mechi bora za watani wa jadi kuwahi kutokea hivi karibuni. Timu zote zikionesha nidhamu kubwa ya mchezo na ufundi mkubwa idara zote.
Mechi ya mzunguko wa kwanza ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika kwa sare ya 1-1 ilitawaliwa na ugomvi mkubwa , kukamiana na kila aina ya karaha hivyo mchezo wa kistaarabu leo umeonesha ukomavu kwa timu zote mbili .
Kimbinu na kiufundi
Tuanze na washindi Simba SC. Mwalimu Joseph Omog aliipigia mahesabu Yanga SC ya kuishambulia muda wote wa mchezo kwa kutumia nguvu kubwa ya viungo wake . Akitumia mfumo wa 4-4-2 ambao mara nyingi katika eneo la kiungo hutumia viungo wawili na sapoti ya mawinga kulia na kushoto kuwachezesha washambuliaji wawili mbele, lakini leo Omog alijaza takribani viungo sita . James Kotei akisimama chini sambamba na Jonasi Mkude , Mohamed Ibrahimu juu , Muzamiru Yassin kama kiungo mshambuliaji na Luizio kama target Man na Kichuya kulia . Wote hawa ni viungo akiwa na mahesabu ya kumiliki mpira , kupanga mashambulizi pia kuikataa Yanga kucheza kati ( direct play )
Kwa kiasi kikubwa Omog alifanikiwa na ndio maana Yanga walipakimbia kati kwa kuweka mpira bali walitumia mipira mirefu kwenda mbele . Muunganiko wa Juma Makapu , Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima ulikosekana na muda mwingi mashambulizi yakijengwa kupitia pembeni kwa wing backs . Heko za pekee kwa Besala Bukungu na Zimbwe Jr ambao leo walikuwa makini kucheza na flanks kwa kupanda kwa tahadhari baada ya kugundua Yanga wanatumia long balls pembeni kufika mbele .
Simba SC ilishindwa kuamua matokeo ndani ya dakika 90 licha ya kuonekana kuizidi Yanga eneo la kiungo kutokana na sababu zifuatazo kimbinu;
Muingiliano wa James Kotei na Jonasi Mkude katika kuisukuma timu mbele . Walijikuta muda mwingi wanasimama Sambamba na kuvunja ile link yao na Muzamiru Yassin ambaye akajikuta leo anadhurura tu uwanjani . Kujipanga vibaya kuliwafanya Makapu na Kamusoko wakisaidiwa Deusi Kaseke aliyekuwa anavunjikia kati kuzima mipango yao ya kushambulia kitu ambao kilikuwa kina mtesa Juma Luizia kupata mipira . Kotei alihitaji sana kuweka mpira chini na kushambulia kwa kasi lakini wenzake walikuwa na tension kubwa na kujikuta wanaingiliana . Kanikosha kwa mbinu zake .
Mpango wa kupitia Pembeni ulikuwa mgumu kwa aina ya uchezaji wa Simba ambao hawana Sprinters wazuri kwenye wings . Wanahitaji give and go passes kwenda mbele .
Lakini pia kukosa utulivu kwenye final third kumeigharimu Simba . MO Ibrahimu , Muzamiru na Juma Luizio walikuwa wanafika langoni bila mipango pia uchoyo na papara za kufunga . Viungo wa kati kucheza nyuma sana kuliwafanya viungo na walinzi wa kati wa Yanga kuelewana vyema na kuzuia " pressing " mahesabu ambayo Omog aliyahitaki sana kwa kujaza viungo.
Tukija kwa Yanga SC nitoe kongole kwa benchi la ufundi la Yanga SC kwa kuifanyia mabadiliko makubwa timu hiyo baada ya kupoteza 4-0 dhidi ya Azam FC . Mabadiliko kimbinu na kiufundi.
Yanga leo imeonesha nidhamu kubwa ya mchezo kwa dakika zote 90. Kitendo cha kuiheshimu Simba na kuichukulia tahadhari ndio kimewapelekea kutoka salama ndani ya dakika 90 na kwenda kupoteza kwenye matuta.
Mechi na Azam FC tatizo kubwa lilikuwa nafasi ya kiungo , ulinzi na jinsi ya kujipanga golikipa .
Hakukuwa na uelewano mzuri kati ya Andrew Vicent na Kelvin Yondani . Kukatika kwa Zullu na wenzake pia usimamaji mbovu wa Dida langoni kulipelekea maafa.
Mechi ya leo kumekuwa na uelewano mzuri kati ya Dante na Yondani wakiunganishwa vyema Juma Makapu kama deep lying holding midfielder. Uelewano wao uliwafanya washambuliaji na viungo wa Simba kushindwa kuwapita na kuwasukuma nyuma licha ya wingi wao . Heko kwa Yondani kwa kucheza jihadi hasa kama mtu wa mwisho kwenye marking.
Dida ameokoa magoli ya wazi matatu kwa kujipanga vyema langoni mwake leo . Alikuwa muda mwingi anachukua tahadhari kabla ya mpira kumfikia kitu ambacho kimemfanya kuwa bora leo.
Kugundua mipango ya Simba SC kwenye eneo la kiungo na kuanza kutumia mipira mirefu kushambulia no credit kwa GL ingawa Simba waliwatambua na muda mwingi walikuwa wakipoteza mpira wanarudi nyuma haraka ( zonal marking )
Ni dhahiri Yanga imekosa mtu wa mwisho kukaa na mpira , kushambulia na kuwatengenezea wenzake . Licha ya Haruna Niyonzima kupangwa kama namba 10 lakini ilimpasa kutembea uwanja mzima kujaribu kuifumua midfield ya Simba SC iliyokuwa ikiwazuia kupitisha mipira kati kitu ambacho kiliondoa kombinesheni yake na Amisi Tambwe na kujikuta forward line nzima ikikatika na kutegemea flanks kushambulia kupitia Kaseke , Msuva au full backs Juma na Haji .
Mechi imeamuliwa kwa matuta si mbaya ilistahili baada ya balance kimbinu na kiufundi . Bado Yanga wana jinamizi la Penati . Wanahitaji kuliondoa kwa mazoezi mengi .
Mchezaji bora kwa ujumla katika mchezo huu ni Besala Bukungu beki namba mbili wa Simba SC . Ameonesha ukomavu na faida ya ukongwe kuisadia Simba kwenye marking na kushambulia.
Asanteni

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video