Sunday, April 21, 2013

1
Na Baraka Mpenja
Vinara wa ligi kuu Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam imewaadhibu maafande wa JKT Ruvu katika mechi ya ligi kuu bara uliofanyika uwanja wa Taifa baada ya kuwatungua mabao 3-0  na hivyo kufikisha pointi 56 wakihitaji pointi moja tu kujinyakulia mwari wa ligi kuu Tanzania bara.
Yanga endapo watatoka sare au suluhu katika mchezo wake ujao dhidi ya wagosi wa kaya Coastal union mei mosi mwaka huu uwanja wa taifa watafikisha pointi 57 ambazo timu nyingine haziwezi kufikisha.
Pamoja na ushindi huo klabu ya Yanga ilionesha soka safi kuwanyanyua mashabiki wake vitini huku wakishangilia kwa staili ya kuua mtu.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Orden Mbaga, hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kambani na winga mwenye kasi kali na umakini mkubwa Simon Msuva.
Hata hivyo, baada ya bao hilo, wachezaji wa JKT Ruvu walimfuata mshika kibendera namba mbili, Lulu Mushi wakilalamikia bao hilo, wakidai lilitokana na maamuzi yasiyo ya haki ya mdada huyo.
Walilalamika mpira waliopewa Yanga warushe walistahili kurusha wao, JKT kwani aliyeutoa ni mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Kiiza Diego.
Kipindi cha pili, Yanga SC walirudi na moto zaidi na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi, yaliyofungwa na Hamisi Kiiza dakika ya 59 na Nizar Khalfan dakika ya 64. 
Katika mchezo wa leo, Yanga SC iliongozwa na kocha wake Msaidizi, Freddy Felix Minziro ambaye alisema bosi wake, Mholanzi, Ernie Brandts anaumwa Malaria.
JKT iliendelea kuongozwa na Kocha Msaidizi, Azishi Kondo na kocha mpya, Kenny Mwaisabula aliyetarajiwa kuanza kazi leo, hakuonekana uwanjani.
Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Said Mohamed dk 86, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan/Said Bahanuzi dk90, Hamisi Kiiza/Jerry Tegete dk82 na Simon Msuva.
JKT Ruvu; Shaaban Dihile, Hassan Kikutwa/Sosstenes Manyasi dk77, Stanley Nkomola, Ramadhani Madenge, Damas Makwaya, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Ally Mkanga/Charles Thadei dk78, Mussa Mgosi, Zahor Pazi na Haroun Adolph.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video