HATIMA ya nafasi ya pili msimu huu huenda ikajulikana leo
wakati Simba inatarajia kuikaribisha Azam fc katika mechi ya ligi kuu Tanzania
bara itayopigwa leo jioni uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Azam wapo nafasi ya pili kwa pointi 45 baada ya kucheza
mechi 23, wakati Simba wanashika nafasi ya nne wakijikusanyia pointi 41
kufuatia kushuka dimbani mara 24.
Kama Simba wanahitaji kuchukua nafasi ya pili wanahitaji
kushinda mechi ya leo ili kufikisha pointi 44 wakisubiri mechi ya mwisho dhidi
ya JKT Ruvu Mei 9 mwaka huu na wakiiombea Azam itoe sare moja na kufungwa mechi
moja.
Baada ya mechi ya leo, jumatano ijayo Azam wanacheza na
Yanga uwanja wa Taifa na watamaliza ligi mei 9 mwaka huu dhidi ya Mgambo JKT
uwanja wa Azam Complex.
Kama Azam watafungwa na Simba halafu wakafungwa na Yanga,
maana yake wataendelea kuwa na pointi 45, Simba 44. Mechi ya mwisho wakishinda
dhidi ya Mgambo, Simba hatakuwa na chake, matokeo pekee yatakayowasaidia Simba
ni kuona Azam anatoka sare na Mgambo baada ya kufungwa mechi mbili.
Kama matokeo hayo yatatokea maana yake Azam atafikisha
pointi 46 ambazo Simba watazivuka kama watashinda tena mechi ya mwisho dhidi ya
JKT Ruvu .
Hivi ni hesabu za nje ya uwanjani, matokea ya mpira wa miguu
hupatikana uwanjani.
Kuelekea mechi ya leo, Simba kupitia kwa afisa habari wake,
Hajji Manara wamesema wanaichukulia kwa uzito wa hali ya juu kuhakikisha
wanavuna pointi tatu.
“Kila mtu anajua umhimu wa mechi hii, tunaichukulia kwa
uzito mkubwa, mechi ni kubwa, tunacheza
na timu nzuri, tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Hakuna mechi rahisi, hata
wateja wetu Yanga inakuwa mechi ngumu lakini mwisho wa siku tunawafunga”.
Amesema Hajji.
0 comments:
Post a Comment