Sunday, April 21, 2013

cheka
Na Baraka Mpenja
Bondia Francis Cheka ametamba kumchabanga mpinzani wake Thomas Mashali ambaye ni bingwa wa uzito wa Middle ukanda wa afrika mashari na kati (ECAPBA) watakapokutana katika pambano la kutetea ubingwa wa afrika mei mosi PTA jijini Dar es salaam.
Akizungumza kutoka mkoani Morogoro alipoweka kambi yake, Cheka alisema yeye hataki maneno mengi ila shughuli ni siku ya pambano ambapo Mashali lazima akione cha mtema kuni.
“Kupitia matndao wa Fullshangwe niwahakikishie watanzania na mashabiki wangu kuwa naendelea kujifua vilivyo hapa Morogoro na nitakapo panda ulingoni wengi wananijua kazi yangu”. Alisema Cheka.
Cheka alisema siku zote maandalizi yake ni mazuri na watu wa Morogoro wanamwamini sana na ndio maana anajiandaa kuwapa raha zaidi siku hiyo.
“Maneno anayoongea Msahali waliongea akian Maugo, Kaseba na wengine, lakini kazi yangu nadhani mnaiona jamani, Mashali haniwezi ingawa mchezo wa masumbwi hauna mwenyewe”. Alijitapa Cheka.
Refarii wa mpambano huo wa kukata na shoka atakuwa ni John Shipanuka kutoka nchini Zambia ambaye alilisimamia pambano kati ya Francis Cheka na Mada Maugo mwaka jana kwa ustadi mkubwa.
Shipanuka ni Afisa Ugavi katika jeshi la Jamhuri ya Watu wa Zambia na ana ujuzi mkubwa wa kusimamia mapambano ya ngumi ya kimataifa.
Aidha, majaji wa mpambano huo ni Daudi Chikwanje kutoka Malawi ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi Cha Malawi na ambaye anakuwa jaji namba moja. Steve Okumu wa Kenya ambaye anakuwa jaji namba mbili na Ismail Sekisambu wa Uganda ambaye anakuwa jaji namba tatu. Msimamizi mkuu wa mpambano huo ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi.
 Hii ni mara ya pili kwa bondia Francis Cheka kutetea ubingwa wake tangu amsambaratishe kwa TKO bondia machachari Mada Maugo katika mpambano uliofanyika mwaka jana mwezi wa Aprili katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video