Friday, April 3, 2015

Mazagazaga ya vyakula waliyonunua Yanga leo kwa ajili ya kujipikia wenyewe nchini Zimbabwe

YANGA imewasili salama nchini Zimbabwe tayari kwa mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho dhidi ya FC Platinum itayopigwa kesho kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Mandava uliopo Gweru Bulawayo.
Yanga walitua kwa ndege maalumu ya Serikali nchini Zimbabwe

Yanga iliifunga Platinum mabao 5-1 katika mechi ya kwanza iliyopigwa februari 15 mwaka huu uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Ili kusonga mbele, Yanga inahitaji sare yoyote ile, ushindi au kutofungwa zaidi ya mabao 3-0.
Kama walijua vile! FC Platinum waliandaa hujuma au fitina kibao za kuwachanganya Yanga.
Yanga wametegeu mtego wa Wazimbabwe kwa kumtanguliza jamaa mmoja 'Kamanda' Samuel Lukumay ambaye ndiye kiongozi anayeiongoza Yanga kukwepa fitina.
Jamaa baada ya kuwasili huko, akachunguza na kugundua kuwa FC Platinum wana mpango wa kuwadhuru kwa kutumia chakula cha Hotelini.
Kamanda wa uhakika Samuel Lukumay (wa tatu kushoto waliosimama, mwenye kofia) alitangulia kubaini fiti za FC Platinum nchini Zimbabwe

Vijana hao wa Robert Mugabe walipanga kutumia dawa za kupunguza nguvu mwilini kupitia vyakula watavyowapa Yanga.
Lakini ukiona ngedere mjini ujue kafugwa! ujanja wao haujaweza kuwaingiza Yanga mtegoni.
Kamanda Lukumay akawadokeza Yanga na kuongoza jahazi la kwenda kununua vyakula wenyewe, mazaga kibao na kujipikia wenyewe na kula wenyewe, raha iliyoje!.
Mpaka sasa Lukumay ndiye baunsa wa timu anayeongoza ulinzi kwenye kambi ya Yanga.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video