Tuesday, April 21, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Simba ililala 2-0 dhidi ya Mgambo katika mechi ya kwanza ya ligi ya Bara msimu huu huku kipa wake mkongwe, Ivo Mapunda, akilambwa kadi nyekundu.'
SIMBA SC ambayo Jumamosi ilifungwa 2-0 dhidi ya Mbeya City FC jijini Mbeya, kesho itakuwa na kibarua kingine kigumu itakapowavaa Mgambo Shooting Stars kutioka Kabuku, Handeni jijini Tanga Uwanja wa Taifa jijini hapa.
Kikosi cha Mserbia Goran Kopunovic cha Sim,ba, kitamkosa kipa kinda Peter Manyika Jr ambaye ana matatizo ya nyonga huku pia akiingia katika mgogoro na uongozi baada ya kuweka maneno yasiyo na tafsida katika ukurasa wake wa Instagram akiwajibu watu wanaomshambulia kwamba ameshushwa kiwango na mtoto wa kike wa mbunge.
Kukosekana kwa Manyika Jr ambaye Jumamosi alifungwa mabao hayo mawili dhidi ya City na kumfanya afikishe mabao 16 katika mechi 22 alizoidakia Simba katika mashindano yote, kunamfanya kipa mkongwe Ivo Mapunda apewe uzi wa Mnyama kukaa langoni kesho.
Hata hivyo, kuwapo langoni kwa Ivo kunaweza kuwa na madhara kwa Simba kesho kutokana na safu ya ushambuliaji ya Mgambo inayoongozwa na Malimi Busungu mwenye mabao tisa kwa sasa sawa na Amissi Tambwe wa Yanga na Abasirim Chidiebere wa Stand United, inamjua vyema Ivo.
Katika mechi yao ya kwanza msimu huu ambayo Simba ililala 2-0 Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Machi 18, Ivo alifungwa bao la kwanza kipindi cha kwanza kabla ya kusababisha penalti na kulimwa kadi nyekundu kipindi cha pili, penalti ambayo Busungu alimtungua Manyika Jr aliyeingia kuchukua nafasi ya Ivo.
Kikosi cha Bakari Shime cha Mgambo Shooting Stars kitaingia uwanjani kesho kikiwa na kumbukumbu tatu mbaya: kwanza kufungwa 2-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Taifa msimu huu, pili kufungwa na Simba kwa kipigo cha fedheha cha mabao 6-0 kwenye uwanja huo msimu uliopita na kupoteza mechi yake iliyopita 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting waliotoka nyuma kwa bao moja na kushinda 2-1 ndani ya dakika tatu (goli la kwanza dakika ya 86 na la pili dakika ya 89).
Simba inapambana kumaliza walau katika nafasi ya pili msimu huu ili ishiriki michuano ya kimataifa baada ya kuikosa kwa misimu mitatu mfululizo. Hata hivyo, nafasi hiyo ni finyu kwa sasa kutokana na kupoteza mechi iliyopita dhidi ya City huku Azam FC wanaowania pia nafasi hiyo wakishinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar Jumamosi na kutanua pengo la pointi kati yake na Simba.
Simba iko nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 35, saba nyuma ya Azam fc na 11 nyuma ya vinara Yanga SC zikiwa zimebaki mechi nne huku Yanga wakiwa wamebakisha tano kabla ya msimu huu kumalizika Mei 9.
Furaha ya Simba kesho itakuwa kurejea kwa kiungo wake mshambuliaji kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, ambaye aliukosa mchezo uliopita dhidi ya City kutokana na kuwa na kadi tatu za njano na pengo lake lilionekana dhahiri katika kikosi cha Wanamsimbazi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video