Na Mahamud Rajab
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga SC jioni hii walishuka dimbani kupepetana na Stand United kutoka mjini Shinyanga na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-2, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Stand United ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la Yanga mnamo dakika ya 20 kupitia kwa Kheri Khalifa mara baada ya beki wa Yanga MbuyuTwitte kufanya uzembe uliotokana na kuruka juu na kuukosa mpira na ndipo kheri akauweka mpira kimiani bila ya ajizi.
Baada ya kufungwa goli hilo Yanga walifanya shambulizi la maana kwa nia ya kusawazisha goli hilo lakini shuti la Ngassa liliokolewa na mlinda mlango wa Stand na kuwa kona.
Haikuishia hapo tu mnamo dakika ya 30 Mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi Amissi Josylin Tambwe aliifungia Yanga bao la kusawazisha baada ya kuiwahi krosi ya Ngassa na kufunga kwa bila ya purukushani yoyote.
Mnamo dakika ya 45, mchezaji wa Stand United Chidiebele alingia kwenye eneo la hatari la Yanga na kuwahadaa mabeki wa Yanga Twitte na Makapu, lakini hata hivyo walifanikiwa kuokoa mpira huo na kuwa kona ambayo hata hivyo haikuwa na madhara kwa upande wa Yanga.
Yanga walijipatia bao la pili mnamo dakika ya 45 kupitia kwa mshambuliaji wake mwenye kasi ya ajabu Mrisho Ngassa mara baada ya kugongeana pasi vizuri na Juma Abdul aliyetokea wingi ya kulia ili kupanda kusaidia mashambulizi kwa timu yake na hatimaye kuzaa matunda ya goli hilo.
Haruna Chanongo alilambwa kadi ya njano mnamo dakika ya 63 baada ya kumfanyia madhambi Mrisho Ngassa.
Stand walisawazisha goli lao dakika ya 64 kupitia kwa huyo huyo Kheri Khalifa baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Chidiebele
Yanga kwa mara nyingine tena waliandika bao la tatu dakika ya 77 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Simon Msuva mara baada ya Amissi Tambwe kuangushwa katika eneo la hatari la timu ya Stand United.
Mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalibaki mabao 3 kwa upande wa Yanga na Stand United 2.
Kwa matokeo ya leo, Yanga wanazidi kuukaribia ubingwa wa ligi kuu msimu huu wakiwa wamejikusanyia alama 49 katika michezo 22 waliyocheza huku wakihitaji ushindi katika michezo miwili tu ijayo ili waweze kujimilikisha taji hilo kwa msimu huu.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa;

Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Mbuyu Twite, Said Juma, Simon Msuva/Hussein Javu dk80, Haruna Niyonzima, Amsi Tambwe, Mrisho Ngassa/Danny Mrwanda dk90 na Andrey Coutinho/Kpah Sherman dk58.
Stand United:
Hamadi Juma, Revocatus Mgunga, Abuu Ubwa, Jisend Mathias, Peter Mutabuzi, John Janga, Hamisi Shengo, Pastory Athanas/Reyna Mgungira dk89, Kheri Khalifa/Chinedu Nwankwoze dk76, Abasalim Chidiebele/Vitalis Mayanga dk89 na Haroun Chanongo.

0 comments:
Post a Comment