Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini TFF iliyokutana Aprili 19, 2015 imepanga kusikilizwa kwa
rufaa ya Damas Ndumbaro Mei 10 mwaka huu, makubaliano ambayo yalifikiwa na pande
zote mbili kwa pamoja.
Kikao hicho kilipitisha taratibu za kisheria ambazo
zitatumika kuamua kesi hiyo, ambazo ni taratibu kama zinazotumika mahakamani
ikiwemo kuwasilisha hoja kwa mdomo na si
maandishi, kitendo ambacho kimekubaliwa na pande zote mbili.
Utaratibu huu umekua ukitumika katika
mahakama za kawaida kuepusha manung'uniko kwa upande mmoja kulalamika umeonewa.
0 comments:
Post a Comment