Friday, April 3, 2015


'Endapo Yanga SC ikifanikiwa kuing'oa FC Platinum, itamenyana na mshindi kati ya Etoile du Sahel FC ya Tunisia na Benfica de Luanda FC ya Angola katika hatua inayofuata ya 16 Bora.'

Wakati Yanga SC imechukua tahadhari kubwa kuelekea mechi ya kesho dhidi ya FC Platinum, ripoti za vyombo mbalimbali vya habari vya Zimbabwe zimeeleza kuwa hali ya hewa ya mji wa Zvishavane, ambao mechi itachezwa, inawiana ya Tanzania — joto na uwapo wa mvua.

Yanga SC, ambayo ilitanguliza mguu mmoja kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuicha FC Platinum mabao 5-1 nyumbani Uwanja wa Taifa jijini hapa mwezi uliopita, inatarajiwa kuingia Zimbabwe mchana huu tayari wa mechi ya marudiano kesho.

Baada ya kutua jijini Harare, Yanga SC, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, wanatakiwa kusafiri kwa basi kwenda Zvishavane.

Viongozi wa Yanga SC waliotangulia Zimbabwe, wamekuwa wanatoa taarifa kuwa kuna mbinu nyingi za kuihujumu Yanga SC ambazo zinapangwa kuhakikisha kikosi cha kocha mkuu Norman Mapeza kinasonga mbele licha ya kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Zaimbwe kukiri kuwa itakuwa ngumu kwake kubadili matokeo na kuing'oa Yanga SC.

FC Platinum itaikaribisha Yanga SC Uwanja wa Mandava na mechi hiyo itachezeshwa na marefa kutoka Angola — Helder Martins de Carvalho, Jerson Emiliano dos Santos na Wilson Valdmiro Ntyamba

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video