Friday, April 3, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Walter Musoma ndiye mpiga faulo hatari wa FC Platinum na ana uwezo mabao yake mengi ni ya mipira ya faulo.'
 
NI kijana mdogo mwenye umri wa miaka 19, lakini shughuli yake uwanjani si ya kitoto. Aliifungia timu yake ya FC Platinum bao la kufutia machozi katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho barani Afrika waliyolala 5-1 dhidi ya wenye Yanga SC Uwanja wa Taifa jijini hapa mwezi uliopita.

Huyu si mwingine, bali ni Walter Musoma, mshambuliaji wa FC Platinum, wapinzani wa Yanga SC katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Mara tu baada ya mechi hiyo kumalizika, nilimfuata mchezaji huyo kupata walau machache kuhusu maisha yake ya soka kabla ya hawajaondoka Tanzania.
 
Mazungumzo yangu yaliyochukua dakika tatu tu yalikuwa hivi:

Mwandishi: Pole kwa kupoteza mechi na hongera kwa goli zuri.

Musoma: Ahsante.

Mwandishi: Leo umepiga mipira miwili ya faulo nje kidogo mwa boksi la wapinzani wenu (Yanga SC) ukafunga bao moja na kugongesha nguzo, nini siri ya upigaji wako huo?

Musoma: Ni mazoezi tu hakuna kingine, kila tukishamaliza programu ya mwalimu ya mazoezi, huwa ninapiga mshuti 10 katika maeneo tofauti tofautio karibu na goli. Hii ndiyo imenisaidia kuwa na shabaha katika mipira ya aina hiyo.

Mwandishi: Hongera, ahsante.

Musoma: Ahsante.

Endapo Yanga SC ikijisahau na kuruhusu faulo nyingi karibu na lango lake, ni wazi mkali huyo wa mipira ya faulo ataiumiza klabu hiyo ya Jangwani kesho.

Uwezo wake ni katika mipira ya aina hiyo nji mkubwa na waliokuwapo Uwanja wa Taifa siku hiyo au kufuatilia video vya mabao yake ya faulo, watakubaliana na mimi kwamba Musoma atakuwa nuksi kwa Yanga SC nchini Zimbabwe kesho.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video