Rooney alifunga goli la juu ya kichwa cha beki mwaka 2011
KWA miaka michache iliyopita, klabu yenye staili ya aina yake duniani, Manchester United haijawa klabu kubwa katika uwanja wake wa nyumbani Old Trafford.
Wapinzani wake wakubwa, Manchester City wametumia pesa zaidi na kushinda zaidi dhidi ya mahasimu wao wa jadi.
Ukweli ni kwamba, United kwa mara ya mwisho kushinda dhidi ya City ni mwaka 2011 ambapo Wayne Rooney alifunga goli kali la juu akipiga mpira juu ya kichwa cha beki na kuipa United ushindi wa 2-1.
Je, Rooney atarudia rekodi hiyo leo United ikiikaribisha City uwanja wa Old Trafford?



0 comments:
Post a Comment