Vikosi vinavyotarajiwa kuanza leo kwenye 'Dabi' ya Manchester
MECHI TATU ZA MANUEL PELLEGRINI 3 v MANCHESTER UNITED 0
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini ana rekodi ya ushindi ya asilimia 100 katika mechi zote 3 alizokutana na Manchester United tangu arithi mikoba Roberto Mancini.
Manchester City 4-1 Manchester United, Septemba 2013
Sergio Aguero alifunga magoli mawili katika ushindi wa kwanza wa Pellegrini katika mechi ya watani hao wa jadi, wakati kocha mwingine aliyekuwa anaiongoza kwa mara ya kwanza United kwenye mechi ya mahasimu, David Moyes alishuhudia Man United ikisambaratishwa.
Manchester United 0-3 Manchester City, Machi 2014
Edin Dzeko alifunga baada ya sekundu 45 tu Old Trafford na baadaye aliongeza la pili na kuifanya City imalize msimu kwa kuichapa Man United mara mbili.
Pellegrini labda anaweza kufikiria kumuanzisha leo Mbosnia huyo.
Manchester City 1-0 Manchester Utd 0, Novemba 2014
Kocha mpya Manchester United matokeo yale yale. Aguero alifunga goli pekee la ushindi.


0 comments:
Post a Comment