
“Namfahamu kocha Phiri (Patrick),
ni kocha mzuri, nilifurahi kufanya naye kazi kipindi nikiwa timu ya Taifa na
yeye akiwa Simba, nina imani kuwa ujio wake utaongeza changamoto kwenye ligi na
ubingwa utakuwa mgumu zaidi msimu ujao,” Maximo
Imechapishwa Agosti 16, 2014, saa 7:06 mchana
BAADA ya kutua nchini, kocha wa Simba Patrick
Phiri alishtuka kusikia Mbrazili Marcio Maximo yupo Yanga na sasa jamaa
amemjibu Phiri akisema: “Ndio nipo Yanga nimejaa tele.” Akaendelea na mambo
yake.
Maximo amesema ushindani mkubwa wa namba ulioko
kwenye kikosi cha klabu hiyo umewafanya baadhi ya wachezaji wanaougua malaria
kutaka kuendelea na mazoezi badala ya kupumzika.
“Namfahamu kocha Phiri (Patrick), ni kocha mzuri,
nilifurahi kufanya naye kazi kipindi nikiwa timu ya Taifa na yeye akiwa Simba,
nina imani kuwa ujio wake utaongeza changamoto kwenye ligi na ubingwa utakuwa
mgumu zaidi msimu ujao,” alisema Maximo
Akizungumzia wachezaji wake, Maximo alisema:
“Ushindani wa namba kwenye kikosi changu umekuwa mkubwa, nafarijika kuona kila
mchezaji anataka kucheza, hiyo inanipa imani kuwa nitakuwa na kikosi bora msimu
ujao.”
Chanzo: Mwanaspoti

0 comments:
Post a Comment