Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 24, 2014 saa 3:00 asubuhi
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano mipya ya
CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea nchini Sudan , Mbeya City fc wanaanza kutupa
karata yao ya kwanza leo hii majira ya 11:30 jioni kwa saa za Sudan dhidi ya Academie
Tchite ya Burundi.
Kuelekea katika mechi hii
itakayopigwa uwanja wa Al-Merreikh mjini Khartoum, ushinidi ni muhimu kwa Mbeya City fc ili
kupata morali ya mashindano haya yaliyoanza jana kwa mechi tatu kupigwa viwanja
viwili tofauti.
Kocha Juma Mwabusi ameiambia MPENJA BLOG kwa njia ya simu
kutoka nchini Sudan kuwa kikosi chake kipo salama na kipo tayari kwa ajili ya
mechi ya leo jioni.
“Tumewasili salama mjini Khartoum. Tulichelewa kufika
huku ili angalau kuzoa hali ya hewa. Lakini haimaanishi hatuwezi kushindana.
Sisi tumejiandaa vizuri na tulikaa Dar kwenye joto ingawa hailingani na Sudan”.
“Mashabiki wetu wawe na imani na timu yao. Tunaiwakilisha
nchi na tutapambana kwa nguvu zote. Wachezaji wana morali ya kufanya vizuri”.
Alisema Mwambusi.
Mbali na mchezo huo wa jioni, mechi nyingine ya usiku
itakuwa baina ya AFC Leopard ya Kenya dhidi ya Enticelles ya Rwanda.
Katika mechi zilizopigwa jana, kwa mujibu wa msemaji wa
CECAFA Rodgers Mulindwa, Victoria University ya Kenya iliilaza Malakia FC ya
Sudan kusini bao 1-0.
Wenyeji Al-Merreikh waliibuka na ushindi mnono wa mabao
3-0 dhidi ya Polisi ya visiwani Zanzibar.
Nao Al-Shandi waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya
Dkhill ya Djibouti
0 comments:
Post a Comment