
Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 24, 2014, saa 4: 24 asubuhi
TIMU
ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (Ngorongoro Heroes)
inatarajia kushuka dimbani leo jijini Kaduna katikati ya Nigeria katika mchezo
wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria (Flying Eagles).
Ngorongoro
wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-0 katika mechi ya
kwanza iliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita.
Kocha
mkuu wa timu hiyo, John Simkoko anahitaji kuiongoza Ngorongoro kupata ushindi
wa mabao 3-0 ili kusonga mbele, au mabao
2-0 ili vijana wajaribu bahati yao kwenye mikwaju ya penati.
Kocha
Simkoko alikaririwa akiwa jijini Dar es salaam akisema bado kikosi chake kina
matumaini ya kufanya vizuri licha ya kimahesabu kuonekana ni ngumu kwa Ngorongoro
kufuzu hatua inayofauta.
Nigeria
walionesha kiwango kikubwa katika mchezo wa kwanza na walitawala maeneo yote. Walioneokana
kujiamini, kumiliki mpira na kucheza kama wapo uwanja wa nyumbani.
Waliwazidi
Ngongoro uzoefu na walitumia vyema makosa ya vijana wa Tanzania.
Nigeria
ni moja ya nchi zinazotisha kwa soka la vijana barani Afrika, lakini kwenye
mpira wa miguu lolote linaweza kutokea.
Cha
msingi vijana wa Ngorongoro wasikate tamaa mapema na kuona mambo hayawezekani.
Wacheze kwa nguvu na kuamini kuwa wanaweza kufunga mabao 3-0.
Mechi
ya ugenini itakuwa na presha kwa timu ya Tanzania, lakini Simkoko ni mwalimu
mzoefu na anaweza kuwatuliza vijana wake.
Mwamuzi
Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Atasaidiwa na Issa
Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni
Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.
Kila
la kheri Ngorongoro Hereos katika mchezo wenu wa leo.
0 comments:
Post a Comment