
Hapa dole tu: Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuitumia Real Madrid katika mchezo wa fainali ya UEFA kesho.

Hakuna tatizo: Ronaldo alifanya vizuri mazoezi leo ijumaa kwa mujibu wa kochaCarlo Ancelotti


Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 11: 15 usiku
MWANASOKA
bora wa dunia, Cristiano
Ronaldo anatarajia kuiongoza Real Madrid katika mchezo wa fainali ya
UEFA kesho jumamosi dhidi ya mahasimu wao wa jiji, Atletico Madrid,
amesema kocha Carlo Ancelotti.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Ureno hajacheza tangu alipopata majeruhi katika
sare ya 1-1 dhidi ya Valladolid mei 7 mwaka huu, na alitarajiwa kucheza
katika mechi ya mwisho ya La Liga dhidi ya Espanyol, lakini aliondolewa
katika kikosi ikiwa ni tahadhari ya mchezo wa kesho wa UEFA.
Hata
hivyo katika mazoezi ya leo mjini Lisbon, Ronaldo ameonekana kama hana
tatizo lolote, hivyo kesho atapambana kutafuta ubingwa wa 10 wa UEFA kwa
Real Madrid.
'Mazoezi ya leo ni muhimu sana. Nadhani Ronaldo hana tatizo lolote". Alisema Ancelotti katika mkutano na waandishi wa habari leo ijumaa.
0 comments:
Post a Comment