Sunday, July 21, 2013


ng'ombe2
Na Gladness Mushi, Ngorongoro
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA)imefanikiwa kutoa Ngombe 20 wa kisasa wenye thamani ya zaidi ya milioni 20 kwa vijiji vinne vya Wilaya ya Karatu kwa madhumuni ya kuendeleza Uhifadhi wa maliasili ndani ya Vijiji hivyo.
Akiongea na waandishi wa habari mapema wiki hii Afisa Ugani wa Mamlaka hiyo ambaye ni Bw Salustin Hallu alisema kuwa huo ni moja ya miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo.
Alisema kuwa mradi huo ambao hapo awali ulianza rasmi na Ngombe wa kisasa 20 uliweza kuwa na manufaa makubwa sana kwa Vijiji vya Troma, Ayalabe, lositete,na Upperutele ambapo hapo awali baadhi ya wafugaji kwenye vijiji hivyo walikuwa wanalazimika kuchunga ndani ya hifadhi
Alifaafanua kuwa mpaka sasa zaidi ya familia 98 kwenye mradi huo tayari wameshanufaika kwa kuwa kila familia moja sasa ina ngombe wa
kisasa mmoja na lengo halisi likiwa ni kuhakikisha kuwa kila familia inajijengea uwezo wa kuchunga ndani na wala sio kutoa mifugo kwenda
kutafuta malisho nje.
Awali alisema Mamlaka pia bado ina mkakati mbalimbali wa kuhakikisha kuwa wanaweza kufikia familia zote sanjari na kuwapa elimu mbalimbali juu ya umuhimu wa kufuga ndani laki ni pia kuwapa mbinu imara ambazo zinatakiwa kutumiwa na wafugaji wa kisasa zaidi
Akiongea kwa niaba ya familia 98 ambazo zimenufaika na mradi huo wa ngombe wa kisasa kutoka Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro bi Emirita Martin alidai kuwa pamoja na kuwa wamepata Ngombe lakini bado Mradi huo unapaswa kuongezewa ngombe ambao wataweza kuwanufaisha wanawake.
Bi Emirita alibainisha kuwa kama kila Boma na familia zitapa Ngombe mmoja ambaye atazaliana basi wakina mama wataondokana na dhana ya kuwa tegemezi kwenye maisha ya kifamilia kwani ufugaji unabadilisha maisha duni na maskini ambayo wanayo baadhi ya wanawake katika Wilaya hiyo ya Karatu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video