Kiwanda Cha Ayalable Dairy kilichopo katika Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha kinakabiliwa na changamoto ya usafiri hali ambayo inasababisha waweze kupokea maziwa lita 800 kwa siku badala ya lita 1500 kwa siku moja kutoka kwa wafugaji jambo ambalo wakati mwingine linasababisha hasara kubwa sana kwa wafugaji pamoja na matumizi mabaya ya maziwa.
Akiongea na Waandishi wa habari wiki hii wilayani humo mtaalamu wa maziwa wa wilaya hiyo ambaye ni Care Elias alisema kuwa changamoto hiyo inasababisha madhara makubwa sana kwa wafugaji.
Alifafanua kuwa hapo awali walikuwa wanapata maziwa machache sana kutoka kwa wafugaji lakini kwa sasa maziwa ni mengi sana katika wilaya hiyo ya Karatu ingawaje sehemu nyingi sana zenye maziwa bado zipo
mbali na eneo la mji hali ambayo inasababisha maziwa yashindwe kufika katika kiwanda hich
mbali na eneo la mji hali ambayo inasababisha maziwa yashindwe kufika katika kiwanda hich
Kutokana na changamoto hiyo alidai kuwa maziwa yanayopatikana kwa ajili ya matumizi ya kiwanda ni machache sana ingawaje kwa huko
viijijini zaidi maziwa yanazalisha lakini yanashindwa kufika kiwandani.
viijijini zaidi maziwa yanazalisha lakini yanashindwa kufika kiwandani.
Akiongelea hali ya uzalishaji wa maziwa katika Wilaya hiyo ya Karatu alidai kuwa uzalishaji wa maziwa umeongezeka sana tofauti na Miaka ya nyuma ambapo Wilaya hiyo ilikuwa inapata maziwa kidogo sana.
Alisema kuwa kwa sasa kiasi cha lita zaidi ya elfu nne kinazalishwa na wafugaji wa Wilaya hiyo ya Karatu lakini hapo awali kiasi cha lita
elfu moja pekee ndicho kilichokuwa kinazalishwa hali ambayo wakati mwingine ilikuwa inasababisha uhaba wa maziwa

Alimalizia kwa kusema kuwa pia kituo hicho kilijengwa kwa ufadhili wa Mamlaka ya Ngorongoro hivyo basi ili kuweza kuokoa kiasi kikubwa cha maziwa ambacho kinapotea kila siku ni vema kama mamlaka hiyo ingeweza kuangalia upya tena namna ya kuwapa gari ambalo litaweza kubeba maziwa hayo kutoka Vijijini zaidi na kuleta katika kiwanda hicho cha Ayalabe
0 comments:
Post a Comment