Sunday, July 21, 2013


Maonyesho ya Ng`ombe Nane nane 2011 (11)
Na Gladness Mushi , Karatu
Zaidi ya wafugaji 600 kutoka katika vijiji vitatu Wilayani Karatu Mkoani Arusha wamefanikiwa kupewa elimu juu ya ufugaji bora wa ngombe sanjari na usafi wa maziwa huku lengo halisi likiwa ni kufanya maziwa ya ngombe yanayotoka katika wilaya hiyo yawe na kiwango kinachokidhi haja za masoko ya maziwa duniani
Hayo yalielezwa na Bw Care Elias ambaye ni mtaalamu wa mifugo sekta ya maziwa katika Wilaya ya Karatu wakati akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema kuwa wafugaji hao walifanikiwa kupatiwa mafunzo hayo kwa vipindi tofautotofauti ili waweze kufanya maziwa yanayotoka katika eneo hilo yakidhi viwango vinavyoitajika
Alisema kuwa wamefanikiwa kupewa mafunzo hayo na wataalamu mbalimbali wa wilaya hiyo ya Karatu ambapo mpaka sasa mafunzo hayo yamefanikiwa kuzaa matunda ingawaje bado sekta ya maziwa inakabiliwa na changamoto nyingi.
Wakati huo huo alidai kuwa kupitia mafunzo hayo ambayo ni endelvu kwa wafugaji wa eneo hilo pia yameweza kuwasaidia wafugaji wa ngombe kuachana na tabia ya kulalamika ovyo kwani wengi wao walikuwa wanazalisha maziwa katika mazingira machafu lakini pindi wanapoambiwa waliona kama wanaonewa wivu.
Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kuwa Halmashauri ya Karatu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya
ngorongoro(NCAA)wamekuwa wafadhili wakubwa sana kwenye sekta ya maziwa lakini bado wanatakiwa kuangalia changamoto mbalinmbali ambazo zinaikabili sekta hiyo kwani kama changamoto zitatuliwa kwa haraka sana basi hata kiwango cha maziwa nacho kitaongezeka

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video