Saturday, July 20, 2013


Simba Vs URADSC_0737Picha kwa hisani ya Mtandao
Na Baraka Mpenja 
Wekundu wa Msimbazi Simba wamekumbana na kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa wakusanyaji wa mapato wa Uganda, klabu ya URA, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dimba la taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo uliokuwa maalumu kwa kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni “King Mputa” Simba walikuwa wa kwanza kuandika bao kimiani kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Betram Mombeki
Simba walionesha kandanda safi kipindi chote cha kwanza wakionana kwa pasi murua, huku safu ya ulinzi chini ya askari raia wa Uganda, Samuel Ssenkoom ikicheza kwa umakini mkubwa.
Kipindi cha pili Simba walianza kwa kucheza soka safi, lakini mambo yakawageukia baada ya mshambuliaji wake Mombeki kuzawadiwa kadi nyekundu kutokana na kosa la kumpiga kiwiko mlinzi wa URA, Jonathan Mugabi katika dakika ya 52, hivo kuwalazimu Simba wenye uchovu wa safari kucheza wakiwa pungufu.
URA waliandika kimiani bao la kusawazisha katika dakika ya 60 likifungwa ma Lutimba Yayo aliyeunganisha krosi maridadi ndani ya eneo la sabule la Simba iliyochongwa na Derick Walullya ambaye aliwahi kucheza Msimbazi na kutemwa kwa madai ya kuwa na kiwango kidogo.
Wakati Mnyama akitafuta kuongeza bao la pili, Yayo tena katika dakiak ya 75 aliiandikia bao la pili URA na kuwanyong`onyesha mashabiki wa Simba waliofurika kuitazaman timu yao ili kesho wapate cha kuongea mbele ya mtani wao, lakini mambo yamekuwa mabaya huku wakiwaombea mabaya Yanga hapo kesho.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, mtandao huu huu umepata nafasi ya kuzungumza na mjumbe wa kamati ya ufundi ya klabu ya Simba na kocha wa soka, John William “Del Piero” ambaye kwa upande wake amesema kikosi cha Msimbazi kimecheza soka safi licha ya kupoteza mchezo huo.
“Simba imecheza vizuri sana, kuna makosa madogo madogo ambayo mwalimu wetu atayafanyia kazi. Pia wachezaji walisafiri safari ndefu sana, wamewasili Dar es salaam alfajiri ya jana, hawajapumzika vya kutosha ila wamejituma na kuonesha soka safi”. Alisema Piero.
Kocha huyo alisema jumatatu kikosi cha Simba kitaingia kambini kujiandaa na tamasha la Siku ya Simba “Simba Day” linalofanyika kila mwaka.
Wakati Simba wakifungwa leo, Yanga nao kesho watakuwa na kibarua kizito mbele ya URA, lakini Afisa habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto amewatoa hofu mashabiki  kwani wamejiandaa vziuri na wachezaji wote wapo salama.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video