Saturday, July 20, 2013


MMG27292Na Baraka Mpenja
Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars, Mdenmark Kim Poulsen amelazimika kutumia muda wake mwingi kupandisha morali ya wachezaji wake waliokuwa na dalili ya kukata tamaa ya kupata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda, “The Cranes” katika uwanja wa taifa wa Nelson Mandela, Namboole jijini Kampala kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN.
Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF, Boniface Wambura Mgoyo amezungumza naFULLSHANGWE na kueleza kuwa wachezaji wa Stars walishaanza kukata tamaa, hivyo imemlazimu kocha Kim kukaa nao kitako na kuwaeleza kuwa katika soka kila kitu kinawezekana, na Uganda wanaweza kufungika tu wakiwa kwao.
“Unajua matokeo ya mechi ya Dar es salaam ambayo Stars walifungwa bao 1-0 yaliwavunja moyo wachezaji, lakini kwa sasa morali yao imepanda sana kutokana na juhudi kubwa ya kocha kim kuwapa ushauri na kuwatia moyo kuwa wanaweza kufanya maajabu”. Alisema Wambura.
Wambura alisema kambi ya Stars jijini Mwanza inaendelea vizuri na wachezaji wanaendelea kuimarika zaidi kujiandaa na mchezo dhidi ya Uganda.
Afisa habari huyo alisema kuwa Star inatarajia kukwea pipa kuelekea Kampala mnamo Julai 24 mwaka hu.
Wambura alisisitiza kuwa mashabiki wa soka nchini wanatakiwa kukubali kuwa soka lina matokeo matatu, kufunga, kufungwa, kutoa suluhu ama sare, hivyo kufungwa kwa stars katika uwanja wake wa nyumbani haimaanishi wameshatoka.
Taifa Stars inahitaji ushindi wa zaidi ya bao moja kwa bila ili kufuzu fainali za kombe la CHAN, lakini makocha na wadau wengi wa soka wanakiri wazi kuwa kuwafunga Uganda Namboole ni kazi kubwa sana na jitihada za makusudi zinatakiwa kufanyika kwani “The Cranes” siku zote wamekuwa wagumu sana kupoteza mechi katika uwanja huo wa Taifa.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video