Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mashetani wekundu, Manchester United wamewaibukia tena Barcelona na dau la pauni milioni 30 ili kuwauzia kiungo nyota Cesc Fabregas ikiwa ni saa chache baada ya David Moyes kufurahia ushindi wa kwanza akiwa kocha mkuu wa United.
Lakini mabingwa hao wa soka nchini Englnad watalazimika kuwa na subira kwani kwa sasa Barcelona wanasubiri kuteuliwa kwa kocha mkuu wa wazee hao wa Katalunya baada ya kocha mkuu Tito Vilanova kujiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.
Wiki iliyopita, United walituma ofa ya pauni milioni 26, ili kusajili Fabregas, lakini Barca walitupilia mbali na kudai hauzwi.
Moyes anatamani kufanya usajili mkubwa wa kwanza tangu amrithi Sir Alex Ferguson, lakini jana alifurahia kuiona timu yake ikipata ushindi wa kwanza baada ya kijana kinda Jesse Lingard na Danny Welbeck kutupia mawili kwa kila moja, huku Robin van akitupia msumari wa tano na kukamilisha ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya All Stars nchini Australia.
United inatarajia kwenda Japan wiki ijayo kuendelea na ziara yao, lakini Moyes akili yake ikiwa katika usajili baada ya kumkosa Leighton Baines kwa ofa ya pauni milioni 12, pamoja na Thiago alijiunga na Bayern Munich.


Balaa kwa Barca: Tito Vilanova amejiuzulu kuifundiha Barcelona kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kiafya

Bosi wa Manchester United, David Moyes macho yote kwa Fabregas
Ingawa kuna mazungumzo juu ya Gareth Bale ambapo United wamekubali kutoa ofa ya pauni milioni 60, huku Mkurugenzi wa United Ed Woodward akisisitiza kuwa klabu yake inaweza kumnunua mchezaji wa bei yoyote ile, lakini Tottenham wameweka ngumu kuuza bunduki yao hiyo.
Kuondoka kwa Vilanova Camp Nou ijumaa ya wiki hii kutaweka ugumu juu ya kuondoka kwa Fabregas ambaye katika mtandao wake wa Twita aliandika “Ujaaliwe nguvu, Tito. Tuko pamoja nawe, nakuombea sana”.
Barca hawatafanya maamuzi yoyote juu ya wachezaji wake mpaka atakapoteuliwa kocha mpya wa kumrithi Vilanova

0 comments:
Post a Comment