Thursday, April 11, 2013

Wanavuka bahari; Simba SC

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC leo wanaingia kambini katika hoteli ya Bamba Beach Resort, Kigamboni, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Azam FC, Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutoka msafara uliokwenda Kanda ya Ziwa wiki mbili zilizopita, wanaongezeka wachezaji wanne tu, kipa Abbel Dhaira, viungo Mwinyi Kazimoto Mwitula, Mussa Mudde na mshambuliaji Felix Mumba Sunzu Jr. na kufanya idadi ya wachezaji 25 watakaoingia kambini jioni ya leo Kigamboni. 
Zaidi ya hapo ni wale yosso waliopandishwa kutoka kikosi cha pili na wachache waliokuwa kikosi cha kwanza ambao walikwenda Kanda ya Ziwa akina Juma Kaseja, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Salim Kinje, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Mrisho Ngassa. 
Ikiwa Bamba Beach, Simba itafanya mazoezi huko huko hadi Jumapili itakapovuka bahari moja kwa moja kuja Uwanja wa Taifa, kumenyana na Azam.
Habari mbaya ni kwamba, kiungo Jonas Mkude hatacheza Jumapili kutokana na kuwa na kadi tatu za njano, lakini kwa kuwa yupo chipukizi Said Ndemla hapana shaka pengo lake litazibwa.
Simba SC imehamia Bamba Beach, baada ya kufukuzwa Sapphire Court Hotel, Kariakoo, Dar es Salaam ambako walilimbikiza deni hadi kufika Sh. Milioni 28 ambazo sasa wanazilipa kwa mafungu.
Awali ya hapo, Simba SC pia walikimbia deni katika hoteli ya Spice, Kariakoo ambalo lilifika Sh. Milioni 27 na wamiliki wa hoteli hiyo wakazuia gari mbili za klabu hiyo, basi dogo aina ya Hiece na nyingine ndogo aina ya salon ambayo alikuwa anatumia kocha Mfaransa, Patrick Liewig.
Simba SC ni kama imeliweka rehani taji lake la ubingwa wa Ligi Kuu, hadi sasa ikiwa inashika nafasi ya nne kwa pointi zake 35, nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 37, Azam FC 43 na Yanga SC walio kileleni kwa pointi zao 49, zikiwa zimebaki mechi tano ligi kufikia tamati.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video