MSHAURI wa zamani wa vigogo wa Ufaransa,
Paris St Germain amesema klabu hiyo itamsajili Wayne Rooney kutoka
Manchester United mwishoni mwa msimu.
Licha ya kocha wa United, Sir Alex
Ferguson kusema hivi karibuni kwamba Rooney hataondoka Old Trafford
mwishoni mwa msimu, mwanasoka huyo wa kimataifa wa England, ameendelea
kuhusishwa kuhamia kwa matajiri wa Ufaransa, PSG.
Sasa, Michel Moulin – ambaye alifanya
kazi kwa muda mfupi kama mshauri wa PSG mwaka 2008 – amesema mpango wa
Rooney kutua huko upo na utatimia.

Anakawenda Ufaransa: Wayne Rooney ameripotiwa kuwa mbioni kuhamia Ligue 1 kuichezea Paris Saint-Germain

Kifaa kitang'oka: Rooney amekuwa akiichezea Manchester United tangu mwaka 2004 alipojiunga nayo akitokea Everton
0 comments:
Post a Comment