BIN ZUBEIRY ilinadika wiki iliyopita
kwamba Ferguson anataka kutumia Pauni Milioni 47 - ambazo zitahusisha na
kubadilishana na Javier Hernandez ili kumnasa mkali huyo wa mabao wa
Colombia.
Wakati United inashinda 2-0 dhidi ya
Stoke, Ferguson alimpeleka msaka vipaji wake mkuu, Jim Lawlor
kumuangalia Falcao akifunga mabao mawili katika ushindi wa 5-0 nyumbani
dhidi ya Granada.
Kaangalie video chini

Anatakiwa: Radamel Falcao (kushoto) akiichezea Atletico Madrid ikiifunga Granada
Manchester City na Chelsea zote nazo
zimehusishwa kwa kiasi kikubwa kuwania saini ya Falcao, ambaye
amejijengea jina kama mmoja wa wapachika mabao hodari duniani, kwa
kuifungia mabao 56 Atletico tangu ajiunge nayo akitokea Porto mwaka
2011.
Lakini United imepiga hatua kubwa katika
kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ikijiandaa
kumuacha Hernandez ahamie Madrid kama sehemu ya dili hilo.

Anaondoka? Javier Hernandez akiichezea United dhidi ya Stoke Jumapili, lakini anaweza kuondoka
VIDEO Angalia mabao bora ya Falcao
0 comments:
Post a Comment