![]() |
Kiungo nyota Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima `Fabrigas` akiwahadaa mabeki wa Mgambo kwenye moja ya mechi walizokutana siku za nyuma |
Na Baraka Mpenja
Vinara
wa ligi kuu Tanzania bara, vijana wa mitaa ya Jangwani na Twiga Dar
Young Africans tayari wapo jijini Tanga “waja leo waondoka leo”
kujiandaa na mchezo wa kesho wa ligi kuu soka Tanzania bara katika dimba
la CCM Mkwakwani dhidi ya wapiga kwata wa Mgambo JKT.
AKizungumza
kutoka Tanga Afisa habari wa klabu hiyo Baraka Kizuguto, amesema
kikosi cha Yanga kiliwasili jana mkoani humo tayari kwa kuziwinda pointi
tatu muhimu mbele ya maafande hao wa jeshi wanaopigania uhai wa kubakia
ligi kuu msimu huu.
“Wachezaji
wote wapo salama kabisa, hatuna majeruhi hata mmoja hivyo ni wakati
mwingine muhimu kwetu kutafuta ushindi wa ugenini na kuzidi kuwatimulia
vumbi wanaotufuata nyuma yetu katika harakati za kuwania taji la ligi
kuu msimu huu”. Alisema Kizuguto.
Kizuto
aliongeza kuwa mchezo huo ni mgumu sana kutokana na mazingira halisi ya
Mgambo ambao wanapigana kufa na kupona wakihitaji mzigo wa pointi tatu
ili kujiweka mazingira mazuri katika msimamo wa ligi kuu msimu huu ambao
Yanga wanatesa kileleni.
“Ushindi
na lazima, mashabiki wetu wasiwe na hofu na wajitokeze kwa wingi
kushuhudia kikosi bora cha Yanga kilichoweka kambi nchini Uturuki na
sasa kuvuna matunda yake mzunguko huu wa pili wa ligi kuu”. Aligamba
Kizuguto.
Yanga wamebakiza mechi nne tu na kati ya hizo wanahitaji ushindi wa mechi mbili kuanzia ya kesho ili kujitangazia ubingwa.
Mechi
walizobakiza ni ya Coastal unioni uwanja wa Mkwakwani, Ruvu JKT uwanja
wa Taifa, Wekundu wa msimbazi Simba uwanja wa Taifa pamoja na mechi ya
kesho dhidi ya Mgambo.
Kati
ya mechi hizo zilizobaki wanajangwani hao wana kibarua kizito mbele ya
Simba na Coastal kutokana na ubora wa timu hizo, lakini kwa upande wa
JKT Ruvu na Mgambo kuna uwezekano wa Yanga kunyakua pointi kufuatia timu
hizo kufanya vibaya katika mechi zake nyingi.
Wakati
Yanga wakijinasibu kuvuna mzigo wote wa pointi tatu, nao Mgambo JKT
kupitia kwa katibu mkuu wake Antony Mgaya wamesema kuwa watapambana kufa
na kupona katika mchezo wa kesho ili kupata ushindi baada ya kupoteza
mchezo uliopita kwa kufungwa 1-0 na Prisons jijini Mbeya.
Mgaya
alisema wanajua Yanga msimu huu wana timu nzuri lakini hii
haiwaogopeshi kupambana kwani kwenye soka lolote huwa linaweza
kutokomea.
“Mgambo
na Yanga kwa majina hakuna ushindani, lakini soka lina maajabu yake,
tunaweza kushinda na kuwashangaza wengi, Kocha Kampira amewaandaa vijana
kwa ajili ya ushindani”. Alisema Mgaya.
Mgambo
JKT wapo nafasi ya 10 wakijikusanyia pointi 24 na juu yao wapo
wanajelajela Tanzania Prisons wenye pointi 26 ambao kwa upande wao
wanaonekana kujinusuru kushuka daraja msimu huu baada ya mapambano ya
muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment