![]() |
Miss Sinza 2012 ambaye pia ni Miss Kinondoni na Miss Tanzania, Brigitte Alfred mara baada ya kushinda taji hilo mwaka jana. Mchakato wa kumsaka mrithi wa taji hilo utaanza April 26 kwenye ukumbi wa Meeda, Sinza. |
Na Mwandishi Wetu
MAZOEZI
ya warembo watakaowania taji la urembo la Sinza, Miss 2013 yataanza
Aprili 26 kwenye ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori na Lufungila jijini.
Taji
la Miss Sinza linashikiliwa na Miss Tanzania, Brigitte Alfred ambaye
ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia, Miss World
2013 mwezi Agosti mwaka huu.
Mratibu
wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi ya mazoezi
hayo yamekamilika na yatasimiwa na kamati ya maandalizi huku ikitafuta
mwalimu kwa ajili ya kuwanoa.
Majuto
alisema kuwa warembo waliowahi kushiriki mashindano hayo wanaruhusiwa
kuja kutoa sapoti kwa warembo wapya na kamati yao itawapa nafasi ya
kuwafundisha warembo wapya ili kuwapa ‘mbinu’ mbali mbali za mashindano
hayo.
Alisema
kuwa fomu za kuomba kushiriki katika mashindano hayo zinapatikana
kuanzia leo (Ijumaa) maduka ya Zizzou, Sinza Afrika Sana, Meeda, Ofisi
za Miss Tanzania, Ofisi za gazeti la Mwananchi (Tabata) au kwa njia ya
mitandao (blogs), balilemajuto, sufiani mafoto, saluti5 au kutuma kwa
njia ya email, [email protected]
“
Lengo letu kubwa ni kumsaka mrithi taji la Miss Tanzania, Miss Kinondoni
na Sinza, mataji yote hayo yapo katika kituo chetu, tumejipanga kulinda
heshima yetu na tunaamini titafanikiwa kwa heshima ya wakazi wa Sinza,
Kinondoni na Tanzania kwa ujumla,” alisema Majuto.
Alisema
kuwa wanawakaribisha warembo wanaotaka ‘kupata taji’ kuchukua fomu zao
ambazo zinatolewa bure. Majuto pia aliwaomba wadhamini wanaotaka
kujitangaza kupitia mashindano yao wanaruhusiwa kuja kudhamini
mashindano hayo na milango ipo wazi.
0 comments:
Post a Comment