KAMARI inalipa. Baada ya miaka kutumia fedha kibao, kusota, vilio hadi kufika Mahakama Kuu, hatimaye Cardiff City ikiongozwa na mkongwe Craig Bellamy imefanikiwa kurejea matawi ya juu baada ya miaka 51 ya kupotea kwenye soka ya England.
Ilikuwa ni sare ya bila kufungana jana
dhidi ya Charlotn iliyowahakikishia kupanda Ligi Kuu, jambo ambalo kwa
miaka ya karibuni hawakuonekana kuliweza.
Lakini kama ulikuwa una msimu kama waliokuwa nao Cardiff, inawezekana ukasamehewa.

Shangwe: Wachezaji wa Cardiff wakishangilia katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya kupanda Ligi Kuu

Mchezaji wa 12 uwanjani: Mashabiki wa Cardiff wakishangilia kurejea Ligi Kuu


Mvinyo wa furaha: Craig Bellamy akigonga shampeni kwenye chumba cha kubadilishia nguo
VIKOSI VYA JANA
Cardiff: Marshall, McNaughton, Turner, Barnett, Taylor, Noone (Smith 71), Kim, Gunnarsson, Mutch, Bellamy, Gestede.
Benchi: Lewis, Whittingham, Cowie, Conway, Mason, Nugent.
Charlton: Hamer,
Solly, Morrison, Dervite, Wiggins, Harriott, Hughes (Gower 81),
Jackson, Pritchard (Green 88), Kermorgant, Fuller (Obika 81).
Benchi: Button, Taylor, Kerkar, Wilson.
Njano: Fuller.
Njano: Fuller.
Mahudhurio: 26,338
Refa: Scott Mathieson
Cardiff imepanda Ligi Kuu England

Timu hiyo imepanda baada ya kucheza
mechi 43 na kufikisha pointi 84 ikiwa kileleni mwa Ligi hiyo, mbele ya
Hull City yenye pointi 77, Watford 71 na Brighton & Hove Albion
yenye pointi 66.
Ilikuwa ni furaha kubwa jana kwa
uongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo baada ya sare hiyo ambayo
moja kwa moja inawapa tiekti ya kuingia kwenye vita na vigogo msimu ujao
katika Ligi Kuu England.
Hawatamsahau refa Scott Mathieson aliyechezesha mechi hiyo iliyowarejesha Ligi Kuu jana mbele ya mashabiki 26, 338.
Cardiff sasa inawaachia vita ya kuwania nafasi nyingine za kupanda Hull City na Watford.
0 comments:
Post a Comment