Baada ya timu ya taifa ya Chile kutangulia fainali ya Confedaration
Cup hapo jana, hii leo mabingwa wa dunia Ujerumani walikuwa wakipepetana
na Mexico kutafuta mshindi mwingine wa kwenda katika fainali.
Mchezo wa leo ulionekana mapema sana kwamba unaweza kuwa wa upande
mmoja tofauti na wa jana kwani kipindi cha kwanza tu tayari Ujerumani
walitangulia kifua mbele kwa mabao mawili kwa sifuri.
Alikuwa Leon Goretzka akitumia dakika 2 kufunga mabao mawili, alianza
dakika ya 6 na wakati Mexico wanashangaa akwafunga la pili dakika ya 8
kabla ya kipindi cha pili Timo Werner kuifungia Ujerumani bao la 3.
Wakati watu wakiamini huenda mchezo huo ukaisha kwa matokeo ya 3 kwa
0, Marco Fabian aliifungia Mexico na kufanya kuwa 3-1 kabla ya Amin
Younes kuipatia bao la mwisho Ujerumani na matokeo kuisha kwa bao 4 kwa
1.
Matokeo hayo yanawafanya mabingwa hao wa dunia timu ya taifa ya
Ujerumani kukutana na mabingwa wa America Chile katika mchezo mgumu sana
ambao utapigwa siku ya Jumapili kuamua nani bingwa wa Confedaration Cup
mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment