Ni kama vile bibie Antonella mke mtarajiwa wa Messi ameamua kumsamehe
Shakira ambaye ni mpenzi wa Gerrad Pique kwani Pique naye ni moja kati
ya waalikwa katika harusi hiyo, hii inakuja baada ya tetesi kuzagaa
kwamba Pique huenda angetoswa katika harusi hiyo.
Tayari ndege mbali mbali zimetua nchini Argentina zikiwa zimebeba
wachezaji maarufu na marafiki wa Lioneil Messi ambao wamekuja kushuhudia
tukio hilo kubwa kwa nyota huyo ambalo litafanyika katika mji wa
Rosario katika sehemu iitwayo Senta Fe.
Wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona Xavi, Samuel Etoo na Puyol
walikuwa kati ya wageni wa kwanza kwanza kuwasili nchini Argentina
katika tukio hilo lakini pia kiungo wa klabu ya Chelsea Cesc Fabregas na
kiungo wa Barcelona Sergio Bosquet tayari wamewasili.
Wageni watakaofika katika harusi hiyo watalala katika moja ya hotel
ya kifahari sana nchini Argentina iitwayo Pullman Hotel ambayo ina uwezo
wa kupokea wageni 188 na hotel hiyo sio ya kitoto kwani kulala humo
katika chba cha bei rahisi kabisa itakubidi kutoa zaidi ya shilingi laki
3 za kibongo.
Messi na Antonella wametoka mbali sana kwani ukaribu wao ni tangia
wakiwa watoto wadogo na hadi wameamua kufunga ndoa wameshakaa katika
maisha ya ukaribu na kufanikiwa kupata watoto wawili ambao ni Thiago
mwenye miaka minne pamoja na mdogo wake, na sasa ukurasa mpya kati ya
hao wawili unaenda kufunguliwa na wanakwenda kuwa mke na mume.
0 comments:
Post a Comment