Bado tu vita ya usajili inaendelea na kila kukicha kumekuwa na vichwa
vya habari vipya huku kila timu ikijaribu kumnunua mchezaji mpya ili
kuimarisha vikosi vyao.
Suala la Alexis Sanchez bado ni suala linalopasua kichwa watu wengi
kwani hawajui kama atabaki Arsenal, ataenda Chelsea, Man City au
atahamia Bayern Munich.
Lakini sasa Bayern Munich ambao kwa siku za karibuni wamekuwa
wakihusishwa sana na Sanchez wameamu kutoa duku duku lao la moyoni
kuhusu masuala ya usajili.
Bayern wanasema wao sera zao kwa wakati wote ni kununua wachezaji
makinda kati ya umri wa miaka 20 hadi 22 na hiyo ndio namna
wanavyoijenga klabu yao.
Lakini wakasema hawako tayari kutumia oesa ndefu sana kwa ajili ya
kununua aina ya wachezaji ambao umri wao umeenda sana ba kufikisha miaka
29 hadi 30.
“Huwezi ukajenga timu kwa usajili wa €100m tena kwa mchezaji ambaye
umri umekwenda hadi miaka 29, hiyo siyo sera yetu” alisema Uli Hoeness
ambaye ni raisi wa klabu hiyo.
Japokuwa Hoeness hakumtaja mtu moja kwa moja lakini inafamika Bayern
walitajwa kumtaka Sanchez ambaye ana miaka 29 na bei yake ni kubwa sana.
0 comments:
Post a Comment