Nohodha wa Sweden na mshambuliaji tegemeo wa PSG Zlatan Ibrahimovic ameandika kwenye akaunti yake ya Facebook post iliyowashtua watu wengi hasa mashabiki wa PSG, baaada ya kusema kuwa mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Nantes ndiyo utakuwa wa mwisho kwake kuwatumikia vigogo hao wa Ufaransa.
Nguli huyo wa soka ambaye anasifika kwa uwezo wake mkubwa uwanjani huku akicheza kwa kujiamini kulikopitiliza, ameweka post hiyo huku taarifa zikidai kuwa atarejea baadaye klabuni hapo kwa shughuli nyingine ya ukocha.
My last game tomorrow at Parc des Princes. I came like a king, left like a legend pic.twitter.com/OpLL3wzKh0— Zlatan Ibrahimović (@Ibra_official) May 13, 2016
Akimaanisha kwamba: Mchezo wangu wa kesho kwenye dimba la Parc des Princes utakuwa wa mwisho kwangu. Nilikuja hapa kama Mfalme na ninaondoka nikiwa kama Legend (nguli)
Zlatan (34) alijiunga na PSG mwaka 2012 akitokea nchini Italy kunako klabu ya AC Milan, na kunyakua mataji manne ya Ligi kuu nchini humo maarufu kama Ligue 1, na kujiongezea hazina ya makombe katika kabati lake, japokuwa watu wengi amekuwa wakitilia shaka ushindani mdogo uliopo kwenye ligi hiyo.
LA Galaxy ya nchini Marekani kutoka Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Major Soccer League (MLS), inatajwa kuwa kwenye mbio za kumwania nyota huyo huku vile vile vilabu kadhaa vya nchini China, England na Mashariki ya Kati vikitajwa kuwania saini yake.
Kocha wa Sweden Erik Hamren anaamini kwamba Zlatan bado ana uwezo mkubwa wa kucheza hata kwenye ligi ya England licha ya umri wake kuwa mkubwa.
"Ana umbo la kuvutia,"alisema. "Endapo Zlatan anapewa fursa ya kucheza, basi ataweza kubaki kwenye klabu kubwa ulimwenguni kwa miaka kadhaa mbele."
0 comments:
Post a Comment