Friday, May 13, 2016

WAKATI Yanga wakiendelea kujinafasi kwenye michuano ya kimataifa, wanaweza kujikuta wakipata pigo kubwa kutoka kwa wapinzani wao wa jadi Simba kuonekana kuanza kuigomea adhabu ya Shiriksiho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hadi sasa Simba haijafanya lolote kuhusu deni la aliyekuwa mchezaji wao Donald Mosoti na kama hali iko hivyo maana yake suala hilo linaweza kuathiri ushiriki wao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika katika hatua ya makundi kama Yanga itasonga mbele.
FIFA ilileta barua Tanzania kwa klabu ya Simba na nakala kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikiiagiza Simba kulipa fedha za mchezaji wake wa zamani iliyomuacha Donald Mosoti bila ya kumaliza fedha hizo za usajili na fedha za kuvunja mkataba baada ya kumuacha.
FIFA imeagiza Simba kulipa Sh milioni 64.2 za Kitanzania pamoja na gharama ya kikao cha Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) cha FIFA, kwa kujumlisha fedha zote sawa na Sh milioni 72.
Hivi Simba imepewa siku 30 kulipa fedha hizo endapo hazijalipwa, basi TFF aishushe daraja na kupokwa pointi tatu isipofanya hivyo Tanzania haitashiriki michuano ya kimataifa hali hiyo pia itawakumba Yanga wakifanya vizuri na wakifuzu katika mchezo wao dhidi ya GD Sagrada ya Angola.
BINGWA lilimtafuta Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara, alisema suala hilo limeshamalizwa bila ya kufafanua zaidi.
Pia lilimtafuta mchezaji mwenyewe alisema bado hajapata hizo fedha zake pia tayari FIFA wametoa namba za akaunti zake za benki ambazo Simba wataingiza fedha hizo.
“Wakinilipa niwatume hiyo ‘bank statement’ FIFA kuonyesha wamelipa, pia mimi nikipokea nitawaambia FIFA nimepata, kwa sasa sijapata taarifa zozote,” alisema.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas alisema uamuzi wa FIFA si wa kupuuzwa hivyo wanaitaka Simba kulimaliza suala hilo kabla ya muda huo.
“Unajua suala hili Simba wanatakiwa kulimaza kwa muda waliopangiwa, kwani FIFA hawana mzaha kabisa kama wasipolipa itakula kwetu na sisi kwa hali ilivyo kama hatutachukua hatua maana yake suala hili litatuathiri kama taifa,” alisema.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video