Jana Roberto Martínez alifukuzwa kunako klabu ya Everton baada ya kudumu kwa misimu mitatu. Sasa swali kubwa lililobaki je, ni nani wa kurithi mikoba yake?. Hii ni orodha ya makocha wanne wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba yake Everton.
1. Frank de Boer

Legend huyu wa Ajax amekuwa akihusishwa sana na kujiunga na Everton. Tayari ameshajiuzulu kufundisha Ajax. Hatua hii hii inaongeza ukweli wa Mdachi huyo kujiunga na 'Toffees'. Huku akiwa ameipa Ajax mataji ya manne mfululizo ya Ligi ya Uholanzi maarufu kama Eredivise, rekodi hiyo inampa nafasi kubwa ya kubeba mikoba ya Martinez kunako klabu ya Everton.
2. David Moyes

Moyes ambaye ni raia wa Scotland aliwahi pia kuifundisha klabu hiyo na kudumu kwa miaka 11 kabla ya kuelekea kunako klabu ya Manchester United na Real Sociedad. Licha ya kwamba alishindwa kuonesha makali yake kwenye vilabu hivyo, Moyes ni kocha mzuri na mwenye mahusiano mazuri na klabu hiyo. Pia anapewa nafasi kubwa ya kurudi ili kuja kurejesha heshima ya klabu.
3. Manuel Pellegrini

Kocha huyu raia wa Chile amejijengea heshima kubwa sana kunako ligi ya England licha ya kibarua chake na Manchester City kuisha mwishoni mwa msimu huu na kutoongezewa muda mwingine na nafasi yake kuchukuliwa na Mhispaniola Pep Guardiola ambaye ataanza rasmi kazi mwezi July.
Akiwa na klabu ya Manchester City, Pellegrini amefanikiwa kuleta makombe kadhaa ikiwemo la ligi kuu.
4. Rafa Benitez

Mashabiki wa Everton pengine wanaweza wasiwe na mapenzi ama imani naye kutokana na kufundisha Liverpool siku za nyuma – ambao ni mahasimu wakubwa wa Liverpool.
Lakini uwezo wa mkufunzi huyo raia wa Uhispania si wa kutilia mashaka kutokana na rekodi aliyoweka katika siku za nyuma. Moja ya rekodi zake kubwa ni pamoja na kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Liverpool mwaka 2005 na vile vile kufundisha timu vigogo kama vile Inter Milan na Real Madrid. Kwa ufupi Benitez ni moja ya makocha watakaoisaidi kwa kiasi kikubwa Everton.
0 comments:
Post a Comment