Friday, February 5, 2016

Katika hali inayoonesha huenda kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho kukaribia kujiunga na klabuya Manchester United, kiungo mchezeshaji waklabu ya Manchester United Mhispaniola Ander Herrera ameibuka na kusema anatamani kufanyakazi na Mourinho maarufu kama The Special One.
Herrera ambaye alisajiliwa na kochawa Manchester United Louis VaGaal akitokea klabu ya Atletico Bilbao amesema anawashangaa sana wanaosema kuwa, Mourinho anacheza soka la kuzuia na kubainisha kuwa maneno au mtazamo huo si sahihi kwani Chelsea ya Mourinho iliyochukua ubingwa msimu uliopita ilicheza soka la kuvutiana la kushambulia.
Akiongea katika mahojiano maalumu na gazeti la Marca amesema inachekesha watu wanaosema Mourinho anacheza soka la kuzuia, “anglia Mourinho amecheza Chelsea na wachezaji kama Fabregas, Oscar, Willian Eden Hazard na Diego Costa lakini akiwa na kiungo mkabaji mmoja tu Nemanja Matic, Huo sio mchezo wa kuvutia?”
Au alipokuwa Madrid ambapo timu yake ilishinda kwa rekodi ya magoli ya mwaka “Na mbali na hilo Mourinho ni kocha ambaye hutoa presha kwa wachezaji wake na kujitwisha mwenyewe mzigo walawama hivyo kuwaacha wachezaji wake wakiwa huru na kufanya kazi yao”.
Kauli hii ya Herrera inaongeza mkaa katika moto ambao mpaka sasa Mourinho anayehusishwa na kuchukua mikoba ya mholanzi Louis Van Gaal ambaye amebakiza mkataba wa mwaka mmoja Old Trrafford.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video