Sunday, December 13, 2015

Manchester Ubited imeshindwa kuwafikia vinara wa ligi kuu England baada ya kuchezea kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Bournemouth huku striker wa zamani wa ‘mashetani wekund Joshua King akipiga msumari wa ushindi kwa Bournemouth.
Bounermouth walipata goli la kuongoza kupitia kwa Junior Stanislas mapema kipindi cha kwanza lakini Fellaini aliisawazishia Uniteddakika ya 24 kipindi cha kwanza.
Bournemouth 1
Man United walijikuta wakishindwa kufurukuta mbele ya Bournemouth baada ya Joshua King kukwamisha wavuni goli la pili muda mfupi baada ya timu hizo kutoka mapumziko akiunganisha pasi ya Matt Richie na kuipa ushindi timu yake ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani.
Kikosi cha Van Gaal huenda kikajikuta kikishuka hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi endapo Tottenham itaifunga Newcastle United kwenye mchezo wa Jumapili. Manchester United kwa sasa ipo nfasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza michezo 16.
Bournemouth 2
KIKOSI CHA BOURNEMOUTH: Boruc, Smith, Francis, Cook, Daniels, Surman, Ritchie, Arter (O’Kane 86), Gosling, Stanislas, King (Murray 65)
Subsambazo hazikutumiwa: Pugh, Rantie, Kermorgant, Federici, Distin
Waliofunga magoli: Stanislas dk. 2, King dk. 54
KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED: De Gea, Varela, McNair (Jones 91), Blind, Jackson, Fellaini (Powell 74), Carrick, Mata, Depay, Lingard (Pereira 31), Martial
Subs ambazo hazikutumiwa: Young, Romero, Schneiderlin, Tuanzebe
Aliyefunga goli: Fellaini dk. 24
Matokeo ya mechi zote za EPL zilizochezwa Jumamosi December 12
Norwich City 1–1 Everton 
Crystal Palace 1–0 Southampton 
Manchester City 2–1 Swansea City 
Sunderland 0–1 Watford 
West Ham United 0–0 Stoke City

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video