Tuesday, October 13, 2015

Sam Allardyce na Arsene Wenger wakisalimiana katika moja ya matukio ya mechi walizowahi kukutana.
Sam Allardyce amekiri kuwa alikuwa akifurahi sana pale ambapo alipokuwa akimfunga Arsene Wenger ambaye kwa upande wake anamwita 'mtu mwenye majivuno'.
Meneja huyo mpya wa Sunderland amesema kwamba, kumfunga Wenger siku zote imekuwa ni jambo la furaha sana kwake katika maisha yake ya ukocha.
Wakati akikinoa kikosi cha Bolton, Allardyce mara zote alikuwa akiwapa wakati mgumu makocha wa timu kubwa kama vile Wenger wa Arsenal, Rafa Benitez aliyekuwa Liverpool wakati huo na Sir Alex Ferguson aliyekuwa Manchester United.
Kwa mujibu wa Allardyce inawezekana ni Benitez na Wenger hasa ambao wanaweza kulalamika kutokana na mbinu zake za ufundishaji mara zote ambazo wamekuwa wakikosa ushindi mbele yake.
Akiandika katika kitabu chake kipya kinachojulikana kwa jina la 'Big Sam: The Autobiography', ambacho kwa sasa kinarushwa moja kwa moja na The Sun , Allardyce amesema kuwa mara nyingi Wenger amekuwa si mtu wa kukubali matokeo kwa haraka zaidi.
 Sam Allardyce na Arsene Wenger wakiwa vitani.
"Nilikuwa na furaha sana wakati nikiifunga Arsenal kuliko timu yoyote wakati nilipokuwa nikiinoa Bolton," anasema Allardyce, "Nilikuwa nikiwanyanyasa sana hali iliyosababisha Arsene Wenger atuchukie.
"Kuna wakati ilikuwa ikifikia hatua hataki hata kunipa mkono wakati ule wanatumia uwanja wa Highbury pale tulipotoka suluhu. Nilikuwa nikimshuhudia akichomoa tai yake na kuitupa chini kwa hasira.
"Anachukulia matoke yale kibinafsi sana lakini pia anatabia za majivuno."
Benitez pia alikuwa akimtuhumu sana kwa staili ya uchezaji wao.
Allardyce pia ana la kusema kuhusu Benitez wakati akiwa na Liverpool, ikiwemo fainali ya Ligi ya Mbingwa Ulaya 2005 iliyofanyika jijini Istanbul.
Wakati Liverpoo ikitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kuwangu AC Milan kwa mikwaju ya penati, Allardyce anasema kuwa, matokeo hayo hayakuwa na mchango wowote na mbinu za Mhispania huyo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video