Mlinzi wa pembeni wa zamani wa Liverpool, John Arne Riise ameonesha mapenzi makubwa kwa majogoo wa jiji baaa ya kuonesha Tattoo aliyochora kwenye mguu wake ambayo imeandikwa maneno maarufu ya klabu hiyo 'You'll Never Walk Alone'.

Licha ya kwamba aliondoka Liverpool na kujiunga na AS Roma zaidi ya miaka saba iliyopita, bado klabu hiyo ya Merseyside ipo moyoni mwake na ameendelea kudumisha Slogani yake.
Riise alikuwa beki kipenzi wakati wa Gerard Houllier akifunga magoli katika mechi zote za watani wa jadi wa Merseyside dhidi ya Everton na dhidi ya Manchester United ndani ya miezi tu baada ya kutua Anfield mwaka 2001.

Riise alikuwa moja ya wachezaji wa Liverpool waliotwaa ubingwa wa Uefa Champions League kwa mikwaju ya penalti dhidi ya AC Milan mwaka 2005
0 comments:
Post a Comment