Saturday, July 18, 2015

Olunga ndiye ameichakaza Yanga


MABINGWA wa kandanda Tanzania bara, Yanga wamechapwa magoli 2-1  dhidi ya Gor Mahia katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Kagame iliyopigwa jioni ya leo uwanja wa Taifa, Dar es alaam.

Gor Mahia, mabingwa wa Kenya ndiyo walioibuka na ushindi katika mchezo huo mtamu uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika kipindi cha kwanza.


Lakini Gor Mahia wakazidi kutamba katika kipindi cha pili kwa kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Michael Olunga.


Olunga aliyekuwa akiisumbua ngome ya Yanga tokea kipindi cha kwanza alifunga bao hilo baada ya kuwatoka Kelvin Yondani na Mbuyu Twite.


Yanga walitangulia kupata bao katika kipindi cha kwanza baada ya Gor Mahia kujifunga baada ya krosi ya Donald Ngoma, hiyo ilikuwa dakika ya 5.


Dakika ya 16, Shakava akasawazisha kwa kichwa baada ya Juma Abdul kumuangudha Walusimbi.

Dakika ya 24, Ngoma akalambwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.

Nadir Haroub Cannavaro alikuwa na nafasi ya kusawazisha kwa Yanga baada ya kupiga mkwaju wa penalty, kipa akaudaka.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video