Unakumbuka jinsi Ashley Cole alivyokuwa mwiba kwa Cristiano Ronaldo?
Labda huelewi kwanini tunamuita Cole ni adui wa Ronaldo.
Beki huyo wa AS Roma alikuwa moja ya walinzi bora wa kulia na alikuwa miongoni mwa wachezaji wachache walioweza kumkaba Ronaldo wakati huo anaichezea Manchester United.

Leo Cole amemkumbushia Ronaldo kuhusu maumivu aliyokuwa anampa wakati huo
akiichezea Arsenal na Chelsea baada ya kumzuia Cristiano kufanya mambo yake katika mechi ya kirafiki iliyopigwa leo katika mashindano ya kimataifa ya maandalizi ya msimu.
Real Madrid wametolewa kwa penalti 7-6 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu (0-0).
Cheki Video
0 comments:
Post a Comment