Washika bunduki wa London, Arsenal wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Asia Trophy baada ya kuichapa Everton mabao 3-1 katika mechi ya fainali iliyopigwa leo.
Kocha mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger alikuwa ametulia kwenye benchi huku vijana wake wakionesha kiwango cha hali ya juu katika mechi hiyo ambayo ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya.
Golikipa mpya wa Arsenal aliyesajiliwa kutoka Chelsea majira haya ya kiangazi, Petr Cech amecheza mechi yake ya kwanza na kuokoa michomo ya hatari.
Magoli ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott (22), Saint Cazorla (58) na Mesut Ozil (63).
Bao pekee la Everton limefungwa na Ross Barkley (76) .

Mshambuliaji wa Arsenal, Walcott akiungana na Olivier kushangilia

Golikipa wa zamani wa Chelsea, Petr Cech amecheza mechi yake ya kwanza
0 comments:
Post a Comment