SIMBA imepanga kushusha kifaa kipya chenye ubora wa hali ya juu ili kukata ngebe za watani wao wa jadi, Yanga, wanaoringia mcheka na nyavu wao, Donald Ngoma.
Uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva, umesema baada ya usajili wa Mohammed Fakhi, Peter Malyanzi, Mussa Hassan ‘Mgosi’, Samir Nuhu, Laudit Mavugo na beki Emily Nimuboma, mashabiki wa timu hiyo wajiandae kupokea kifaa kingine.
Alipohojiwa na BINGWA, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema wanamshusha mchezaji mwingine atakayekuwa tishio kama kawaida yao
0 comments:
Post a Comment